Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaapisha Majaji wateule
Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaapisha jumla ya Majaji 14 wa Mahakama ya Rufani (T) na Mahakama Kuu, mmoja akiwa ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na wengine 13 wakiwa Majaji wa MahakamaKuu.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika mapema leo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Rais aliwaapisha Majaji walioteuliwa hivi karibuni.
Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya hafla ya kuwaapis